Kwenye kiwanda kinachotengeneza zile Filamu za dunia ( Hollywood ) Marekani kunazo Nyota nyingine ambazo zina damu nyingi ya Afrika, yani Mastaa ambao wanang’ara Hollywood lakini wana asili au damu ya Afrika. 10 . Lupita Nyong’o Lupita Nyong’o ni Mzaliwa wa Mexico lakini mwenye asili ya Kenya, na ameshinda tuzo za Oscar za mwaka 2013, Movie ya “12 years a slave” ndio iliyompa nafasi ya kushinda tuzo hiyo ambapo pia mwaka 2014 katika jarida la “People ” la Marekani alitajwa kama Mwanamke mwenye mvuto duniani na mwaka 2018 tutarajie kumuona kwenye movie mpya ya black panther. 9. Kandyse McClure Kandyse alizaliwa Durban, Afrika Kusini ambapo kutokana na uzuri wa kazi anazozifanya Marekani amepata sifa na umaarufu mkubwa na kumfanya kuingia katika list ya waigizaji 10 wa kike kutokea Afrika wanaofanya vizuri Hollywood, moja ya kazi zake zilizompa umaarufu ni “Hemlock Graove” ...
Comments
Post a Comment