Waigizaji 10 wa kike wenye damu ya Afrika wanaong’aa Hollywood Marekani

Kwenye kiwanda kinachotengeneza zile Filamu za dunia (Hollywood) Marekani kunazo Nyota nyingine ambazo zina damu nyingi ya Afrika, yani Mastaa ambao wanang’ara Hollywood lakini wana asili au damu ya Afrika.
10. Lupita Nyong’o
Lupita Nyong’o ni Mzaliwa wa Mexico lakini mwenye asili ya Kenya, na ameshinda tuzo za Oscar za mwaka 2013, Movie ya “12 years a slave” ndio iliyompa nafasi ya kushinda tuzo hiyo ambapo pia mwaka 2014 katika jarida la “People” la Marekani alitajwa kama Mwanamke mwenye mvuto duniani na mwaka 2018 tutarajie kumuona kwenye movie mpya ya black panther.
9. Kandyse McClure 

     Kandyse alizaliwa Durban, Afrika Kusini ambapo kutokana na uzuri wa kazi anazozifanya Marekani amepata sifa na umaarufu mkubwa na kumfanya kuingia katika list ya waigizaji 10 wa kike kutokea Afrika wanaofanya vizuri Hollywood,  moja ya kazi zake zilizompa umaarufu ni “Hemlock Graove”
8. Thandie Newton
Thandie Newton amezaliwa November 6 1972 London England lakini ana asili ya kiafrika akitokea Zimbabwe, ameshiriki kwenye filamu ya Mission impossible 2 akiwa na muigizaji maarufu Tom Cruise.
7. Ella Thomas
Mrembo huyu alizaliwa Eritrea na alishawahi kushiriki kwenye tamthilia tofauti za Marekani  ikiwemo CSI NEW YORK na amewahi kuigiza kama mpenzi wa P Diddy katika tamthilia ya “Entourage” , Ella Thomas ameshawahi pia kutumika kwenye majarida mbalimbali kama ya Vogue, Glamour, ELLE, Tiffany na Levis ya Marekani.
6. Megalyn Echikunwoke
Ni Mwigizaji wa Marekani ambae alizaliwa Spokane,Washington huku baba yake akiwa ni mzaliwa wa Nigeria, ameonekana kwenye  “90210”, “The 70s show”,”House of lies” na kwenye tamthilia ya “The 4400”
5. Michelle Van Der Water
Ingawa amelelewa na kukulia Australia, Michelle ni mzaliwa wa Afrika Kusini ambapo baba yake ana asili ya Dutch-African na mama yake akiwa Indian-African, Mrembo huyu ameshiriki kwenye tamthilia ya CastleMelrose Place na NCIS Los Angeles.
4. Liya Kebede
Ni Mwanamitindo/Mwigizaji pekee Mzaliwa wa Ethiopia ambae aliwahi kutajwa na Jarida la FORBES kuwa Model anaeshika namba 11 duniani kwa kulipwa pesa nyingi.
Liya amewahi kutumika kwenye matangazo ya kampuni ya Estee Lauder na pia kwenye makampuni mengine makubwa na amewahi kutokea kwenye majarida ya Victoria Secret, Tommy Hilfiger, Yves Saint -Laurent, Dolce & Gabbana, Louis Vuitton.
3. Gugu Mbatha-Raw
Ukiachilia mbali kuwa ni Mwigizaji, Gugu ana asili ya kiafrika kutokea Afrika Kusini ambapo mama yake anatokea Uingereza na amelelewa na kukulia upende wa mama yake lakini baba yake mzazi Dr Patrick Mbatha anatokea Afrika Kusini.
Jina na umaarufu alionao ni kutokana na vipindi vya TV na Tamthilia.
2. Azie Tesfai
Azie Tesfai amelelewa na kukulia Los Angeles Marekani ambapo wazazi wake wote wawili wana asili ya Ethiopia na Eritrea, umaarufu wake umepatikana kupitia movie ya Jane The Virgin lakini pia ni Mwigizaji mwenye degree ya Business Administration yaani masuala ya utawala katika biashara.
  1. Charlize Theron
Ni Mwigizaji mwenye asili ya Afrika Kusini ambae wengi walimfahamu zaidi kupitia filamu za The Cider House RulesThe devils Advocate na Monster.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzia: Mbunge wa Songea Mjini Gama Kuzikwa Kijijini Kwao Likuyufusi

Dogo Aslay Hizi Sasa Sifa Zimezidi Kipimo..Umetuzalilisha Wanawake